TUNU ISOKIFANI
Kwa fahari najigamba, mataifa natangaza,
Mahari kote natamba, penye nuru hatagiza,
Mnene hata mwembamba, sifa zote namaliza,
Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika.
Chakula changu asili, matunda tele nachuma,
Chastahili kimwili, cha wengine ntalalama,
Kisotiwa kemikali, huwezi tamani tema,
Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika.
Rangi yangu maridhawa, watambua walimwengu,
Rangi ile ya uzawa, na sikama ya kizungu,
Raha nakshi kutiwa, na nyeusi rangi yangu,
Ni...
Continue reading...