Get Your Premium Membership

Tunu Isokifani

TUNU ISOKIFANI Kwa fahari najigamba, mataifa natangaza, Mahari kote natamba, penye nuru hatagiza, Mnene hata mwembamba, sifa zote namaliza, Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika. Chakula changu asili, matunda tele nachuma, Chastahili kimwili, cha wengine ntalalama, Kisotiwa kemikali, huwezi tamani tema, Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika. Rangi yangu maridhawa, watambua walimwengu, Rangi ile ya uzawa, na sikama ya kizungu, Raha nakshi kutiwa, na nyeusi rangi yangu, Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika. Wajiona takataka, kutamani visovyao, Puani vinawatoka, na visokoma vilio, Amakweli waumbuka, vyawakaba kwenye koo, Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika. Nimetulia Mawenzi, mevuka vingi vilima, Ni zamu yao washenzi, mizigo kwa wao mama, Nyuso zenye makunyanzi, watembea kiinama, Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika. Uzuri wa kitu sasa, waja kwa historia, Kosa kurudia kosa, la Ndugu alokosea, Jikinge na hili kosa, na tao kufuatia, Ni tunu isokifani, kuzaliwa Afrika. By MUSSA SHIKOME

Copyright © | Year Posted 2017




Post Comments

Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem.

Please Login to post a comment

A comment has not been posted for this poem. Encourage a poet by being the first to comment.


Book: Shattered Sighs