Sisi Kama Sisi
Tatizo letu sisi kama sisi ni kwamba hatuna elimu lakini ni wajuaji
Tatizo letu sisi kama sisi ni kwamba hatutaki kutembea bali kukimbia
Tatizo letu sisi kama sisi ni kwamba hatushibi,
Tunakula mpaka tunajamba
Tuna ujeuri usiokuwa na faida
Tuna ujeuri usiokuwa wa kawaida
Na tunaona ni sawa tu.
Tatizo letu sisi kama sisi ni wanafiki, Tunasema ndio kumbe tunamaanisha la
Tatizo letu sisi kama sisi ni wavivu, hatuoni maana ya kuchapa kazi, Sio kufanya kazi bali kuchapa kazi Tuna ujeuri usiokuwa na faida
Tuna ujeuri usiokuwa wa kawaida
Na tunaona ni sawa tu.
Tatizo letu sisi kama sisi hatupendani, Tunathamini watu wa nje kuliko wa ndani Chakushangaza hata hawa ndugu zetu kina nyani Huwa wanapeana heshima fulani
Tuna ujeuri usiokuwa na faida
Tuna ujeuri usiokuwa wa kawaida
Na tunaona ni sawa tu.
Sisi kama sisi hatuwezi kuendelea
Maana tayari kizazi chetu kimeshapotea
Wale waliobaki kazi yao kubwa ni kuwaonea na kuwatendea wale wenzao wanao wategemea
Ule ujeuri usiokuwa wa kawaida na faida sasa umebaki kutuzomea
Na tunaona ni sawa tu.
© SMS
Copyright © Shamsa Suleiman | Year Posted 2015
Post Comments
Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem. Negative comments will result your account being banned.
Please
Login
to post a comment