Get Your Premium Membership

Nitaolewa Kesho

Wasema subira yavuta kheri, Kamba iliyovuta kheri yakatika, Yakatika na Uzito wa huba, uliojawa na mahaba, Na safari ya mapenzi, iliyojaza sheheni, Kwake nimetia Nanga, sihitaji kivuko, Nasema hivi, Nitaolewa kesho. Haba na haba hujaza kibaba, Kibaba kilichosheheni mapenzi ya Dhati, Moyo ukafurika, kwa pepo za mapenzi yake, Sihitaji feni zenyu, kwake upepo napata, Nasema hivi, Nitaolewa kesho. Safari ndefu ya mapenzi, iliyojawa machafuko, Chombo alishikilia usukani, captain wa mapenzi, Zake huba haziyumbishwi, kwa nyangumi au papa, Nasema hivi, Nitaolewa kesho. Hayawi hayawini sasa, yamekuwa na kunenepa, Yanini kukondeana, wakati twashibana, Sifurukuti hafurukuti, mapenzi Ndiyo nguzo yetu, Nasema hivi, Nitaolewa kesho. Yalianza kama chemichemi, sasa yafurika kama bahari, Ilikuwa ni bahati, kufurika kwake hivi, MUNGU AKITUJALIA, Hii ya kesho tatimia, NASEMA HIVI, NITAOLEWA KESHO

Copyright © | Year Posted 2019




Post Comments

Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem.

Please Login to post a comment

A comment has not been posted for this poem. Encourage a poet by being the first to comment.


Book: Shattered Sighs