Tutampata Tu
Tutampata tu, tutampata
Kwenye Milima na mabonde tutampata
Kwenye maziwa na mabahari tutampata
Tutampata tu.
Kwenye majiji na mabarabara na manyumba
Kubwa na ndogo,
Tutamsaka na Tutampata
Kwenye mapango na mabonde tutampata tu
Hata kwenye shimo lenye giza na mifereji ya maji taka
Tutampata tu.
Tutampata , tutampata
Chini ya mti na chini ya nuru ya mbalamwezi
Kwenye Jua kali na kwenye milio yamatarumbeta
Tutamsaka, tutampata
Tutampata tu.
© SMS 2015
Copyright © Shamsa Suleiman | Year Posted 2015
Post Comments
Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem. Negative comments will result your account being banned.
Please
Login
to post a comment