Get Your Premium Membership

Shoga Atoka Ulaya

Juzi juzi tulikuwa tunakutana Kwenye mishwari tulipitana Hili na lile tuliambiana Menzangu ukaenda majuu Kufika kule ukajiona wewe mungu Uliotuacha huku nyuma ukatufananisha na vyungu Haya yote yalinifanya nihisi uchungu Lakini usijali siku hadi siku Nitarudisha zangu nguvu. Umerudi jana, kimya kimya unaogopa kurogwa Waache kurogwa wenye mahela Urogwe wewe hombolela Kwa maalim ulifika Dua na ubani ukaoshwa Macho ya watu yasije kukudhuru Maana wewe ni kama nuru Kilaupitapo mwanga unazidi kuwaka Shoga hatukuwezi Huko majuu itabidi tufike Hata kama kukifika kama wezi. Leo tumegongana Excuse me ukanitamkia Kiswahili umesahau Barabara zina vumbi sana Watu huwawezi Uswazi umewazidi Sana wamekuwa wakaaidi Maneno wanayo ongea unaona kwako si sahihi Sana sana unawalinganisha na watu wa chini ?Kila ukimaliza kuamkia Mkono wako unaosha na sabuni Maradhi ya uswazi unayaogopa Usije ukarudi ‘kwenu’ na magonjwa ya kuporomoka Kwa majembe na mashoka Unagamba kama mungu kakupa vyema ya kuokoka Shoga umetisha Huko majuu mwenzagu hatusemi Leo kunisalimia unaona tabu Mila za kwetu kwako unaona kavu Kila usimamapo unahesabu hadi tatu Asije mshenzi kukupora ukahisi moyo umekuwa mchafu Maana huku kwetu wezi kweli ni tabu Shoga tangu umerudi kutoka ulaya, hatukuwezi Nakupa miaka kama kumi Umalize katabia kauhuni Umalize ulaya kuwachuna Uje huku tukucheke Maendeleo uliokuwa unayataka yamekupiga teke Aibu unawakataza kwenu wasipayuke Kwakeli wewe mtoto wa kike Kubali yakubalike Nafsi yako ifanye impumzike

Copyright © | Year Posted 2015




Post Comments

Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem.

Please Login to post a comment

Date: 1/22/2016 9:16:00 PM
SHAMSA, Enjoyed the way you expressed every line. Always with LUV **SKAT
Login to Reply
Date: 12/7/2015 4:23:00 AM
ahsante, do the words have meaning
Login to Reply
Date: 12/6/2015 11:50:00 PM
sounds nice. is it spontaneous expression or a language
Login to Reply
Suleiman Avatar
Shamsa Suleiman
Date: 12/7/2015 4:14:00 AM
Ahsante Francis, It is an expression. Sort of a mirror of how individuals respond to loved ones when they change. A bit of anger, anxiety, jealousy and longing.

Book: Shattered Sighs