Kenya-Ian Munywe
KENYA
Ndege ya unyanyapaa inapaa,
kila siku ni balaa.
Alaa,
alaa!
Hamna kazi,
swali hili ni wazi.
Haya sio maneno tu,
bali ni kilio cha waja.
Wengi wanaodhulumiwa,
kilio ni cha haki!
Tumechoka na uhuni,
unaokiuka kanuni.
Vyakula,
bei ghali!
Maisha yetu yamo mnadani,
dalali mate yanamdondoka!
Sisi sote ni binadamu,
ni wakati.
Tuungane,
tuimarishe nchi yetu.
Kenya,
ni yetu sote.
IAN MUNYWE©
Copyright © Ian Munywe | Year Posted 2018
Post Comments
Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem. Negative comments will result your account being banned.
Please
Login
to post a comment