Hayakuhusu Anayekubusu
Nakwambia ndugu Masanja kwani yanakuhusu anaye nibusu?
Kwani nauliza, lazima nije kwako niombe uniruhusu?
Mwaka Juzi nilijaribu kufanya hivyo, ndani kwako ukanitoa na kisu
Ukawaonya majirani na ndugu wakae mbali na mimi maana akili zangu nusu
Kweli ndugu yangu , leo unataka nije kwako uniruhusu?
Kwani wewe, lini umekuwa wangu mtu?
Wakunisimanga na kulikemea nakula vyako vitu?
Wakati unanipa ulisema hivi vyote vya kwetu!
Angalia tumi macho twako kama chatu
Unaki mbelembele kama fyatu
Sitaomba wala kutaka vyako vitu
Nilijaribu na kuapa sito kuja kuthubutu
Nakwambia Ndugu yangu, hayakuhusu anaye nibusu!
Copyright © Shamsa Suleiman | Year Posted 2016
Post Comments
Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem. Negative comments will result your account being banned.
Please
Login
to post a comment