Get Your Premium Membership

Mwangwi Wa Mapenzi

Katikati ya pango la upweke, Najiona niko na wenge, Kukata tamaa kuongezeka, Fikra nazo kusononeka. Natafuta pa kuponeka, Pango hili kulikwepa, Matumaini kutoweka, Pangoni Niko gizani. Ghafla mwangwi watoka wapi!? Mwangwi huo wataka nini!? Kumbe Mwangwi wa mapenzi, Wanionyesha mwangaza. Mapendano pasi masimango, Ndio jadi ya mwangwi huo, Mapambazuko ya hisia, Pangoni nitoke hapo. Nishakuwa na mapepe, Pangoni siko tena, Mwangwi huo wa mapenzi, Wanishibisha mapenzi.

Copyright © | Year Posted 2019




Post Comments

Poetrysoup is an environment of encouragement and growth so only provide specific positive comments that indicate what you appreciate about the poem.

Please Login to post a comment

A comment has not been posted for this poem. Encourage a poet by being the first to comment.


Book: Shattered Sighs