Hustle Ya Life

Written by: Dan Adimi

Life ni hustle,
Na kama tussle,
Wakati mwingine huumiza moyo.

Kuna kupanda na kushuka,
Kulia na kucheka,
Na kama mchana,
Bingu bila jua,
Baada ya huzuni huja furaha.

Kama soldier,
Imara kusimama,
Machungu ya maisha,
Kama mafuta kwenye kidonda,
Uchungu hutuliza.

Kusonga mbele haimaanishi kusahau jana,
Na masahibu ya jana kuisha,
Haimaanishi kesho hayatarudi.

Kumaanisha? Machozi ya leo,
Kesho ni makumbusho,
Na moyo kuvunjika leo,
Kesho ni ngao, 
Ya kujinasua kutoka kwa mtego.