Ningekua Rais

Written by: Emmanuel Balele

ningekua rais wa nchi hii
Ningewatosa marafiki
Sababu wamekua chanzo cha matatizo
Maishani mwangu kwa miongo
Ningekua rais wa nchi hii
Wageni wangetusifu kwa zetu bidii
Heshima wangetupa
Na sio dharau sasa wanazotupa